
Akitoa neno la shukrani mwenyekiti wa kamati hiyo ya maandalizi sheik Nurdini Kishiki amesema haya yote yamewezekana kutoka na utayari wa nchi kwa maana ya ushiriki wa kila mtu kuanzia mifumo ya ulinzi nz usalama wa nchi,vibali toka kwa taasisi mbali mbali za serikali pamoja utayari wa watanzania.
Aidha amewataka sasa waislam kote nchini kuendelea kutumia mwezi mtukufu wa ramadhani kutafakari makuu ya allah huku akiwataka pia kuzitumia fursa ambazo zimetokana na mashindano hayo ambayo hufanyika kila mwaka katika kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhan.
Sanjari na hilo ametoa shukrani kwa washiriki kutoka mataifa 22 ya Africa huku akiwataka watanzania sasa kujiandaa na mashindano makubwa ya quran ya dunia ambayo yanakwenda kufanyika jumaoili ya tarehe 24.04.22 katikq viwanja vya diamonmdi jubilee