
(Erik Ten Hag Kocha mpya wa Manchester United)
Ten Hag atakuwa kocha mpya wa Man United kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwisho wa msimu huu hadi mwezi Juni 2025, kukiwa na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi na yeye ndiye tumaini la mabadiliko na kuanzisha ufalme mpya katikaviunga vya Old Trafford.
Taarifa rasmi ya Manchester United & Ajax imethibitisha makubaliano hayo kwamba tayari yamesha kamilika na kusainiwa rasmi. Mkurugenzi wa Soka wa Mashetani hao wekundu John Murtough amesema wamefurahishwa sana na maono na mipango ya muda mrefu ya kocha huyo mpya na kuirejesha Man.United kwenye kiwango wanachotaka cha kushindania mataji, Pia ari yake na dhamira yake inaone wazi katika kufikia malengo hayo.
Erik ten Hag mwenyewe anasema: "Ni heshima kubwa kuteuliwa kuwa kocha wa Manchester Utd, ninafuraha kubwa. Ninajua historia ya klabu hii kubwa na shauku ya mashabiki, na nimedhamiria kabisa kutengeneza na kuendeleza timu yenye uwezo wa kuleta mafanikio yanayostahili".
Kocha huyo ana wastani wa ushindi wa asilimia 79 (79%0 akiwa na Ajax kwenye ligi kuu ya uholanzi Eredivisie, na ndiye kocha bora zaidi aliye na michezo zaidi ya 100 akiwa na timu moja katika historia ya ligi kuu ya uholanzi. Erik Ten Hag ameiongoza Ajax katika michezo 210 akishinda michezo 156, akipata sare michezo 25 na kupoteza michezo 29. Ameshinda taji la ligi kuu ya uholanzi Eredivisie 2, Dutch Cup 2 na Dutch Super Cup 1.