Friday , 29th Apr , 2022

Mshambuliaji wa Liverpool MoMohamed Salah amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka 2022. Nchini England na Chamba cha waandishi wa habari za michezo England (FWA). Nae Mshambuliaji wa timu ya wanawake ya Chelsea Sam Kerr ameshinda tuzo hiyo upande wa wanawake.

Salah kafunga mabao 30 msimu huu kwenye michuano yote katika michezo 40

Salah amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa na waandishi wa habari akiwashinda Kevin De Bruyne wa Manchester City na Declan Rice wa West Ham United waliomaliza nafasi ya pili na tatu. Hii ni mara ya pili mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Misri anashinda tuzo hii mara ya kwanza alishinda mwaka 2018

Msimu huu wa 2021-22 ambao bado unaendelea Salah amefunga mabao 22 ndio kinara lakini pia anaongoza kwa kutoa pasi za mabao (Asissts) 13 kwenye Ligi kuu England. Akiisaidia klabu yake Liverpool kufikisha alama 79 wakiwa nafasi ya pili tofauti ya alama 1 dhidi ya Manchester City wenye alama 80 ambao ndio vinara wa EPL. Lakini kwa ujumla msimu huu amefunga mabao 30 kwenye michezo 44 kwenye michuano yote.

Sam Kerr

 

Upande wa wanawake Sam Kerr amepata asilimia 40 ya kura zilizopigwa amewashinda Vivianne Miedema wa Arsenak na Lauren Hemp wa Manchester City. Kerr msimu huu kwenye Ligi ya wanawake amehusika kwenye mabao 22 amefunga mabao 18 na ametoa pasi za mabao 4, na klabu yake ya Chelsea inaongoza Ligi kwa tofauti ya alama 4 dhidi ya Arsenal Chelsea wanaongoza Ligi wakiwa na alama 50. Wachezaji hawa watapewa tuzo zao Mei 5, 2022.