
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla
Aidha RC Makalla amesisitiza maboresho ya miondombinu kufanyika katika masoko yote Jijini Dar es salaam huku akiwataka wananchi kuacha kulilaumu Jeshi la zimamoto kwa kwa kuonekana hawafanyi kazi ipasavyo.
Kwa upande wao Wenyeviti wa masoko ya Mkoa wa Dar es salaam, wametaka zifanyikie juhudi kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia nishati mbadala kama gesi, na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni huku TANESCO wakitakiwa kufanya ukaguzi wa mitambo yao mara kwa mara.
Katika kipindi cha mwaka 2021/ 2022 masoko ya Jijini Dar es salaam yalioungua ni pamoja na soko la Kariakoo, soko la Mbagala, soko la Mchikichini, soko Mwenge la Cocacola na soko maalum la walemavu ilala boma.