Monday , 2nd May , 2022

Watu watano wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mwanza kwa tuhuma za kumuua mwalimu wa shule ya sekondari ya wasichana Bwiru na kisha kuiba vitu mbalimbali vikiwemo Television, Radio pamoja na Pasi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Ramadhan Ng’anzi amesema watu hao walimvamia mwalimu huyo majira ya usiku akiwa amelala na kumchoma na kitu chenye ncha kali.

Katika tukio linguine kamanda Nga’anzi amesema watu 21 kutoka mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mwanza wanashikiliwa kwa tuhuma za kuvunja ghala na kuiba televisheni 167 na kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha Kamanda Ng’anzi amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na idara ya uhamiaji wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 68 kutoka nchi za Ethiopia wenye umri kati ya miaka 14 hadi 25 ambao walikuwa wanataka kuelekea nchi ya afrika kusini.
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limewahakikisha usalama wakazi wa mkoa huo siku ya kesho ambapo watakuwa wanasherehekea sikuu ya eid el fitri.