
Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo Waziri Masauni amelitaka jeshi la Polisi ndani ya siku saba wawe wamewakamata wahalifu hao.
Waziri wa mambo ya ndani Mhandisi Hamad Masauni ametoa siku 7 kwa jeshi la polisi kuwakamata watu wote waliohusika katika matukio ya uvamizi maarufu kama ‘Panya Road’.
Aidha amesisitiza wananchi kushirikishwa zaidi katika maamuzi yanayofanywa na viongozi.
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Simon Sirro amesema kutokea kwa matukio hayo katika maeneo ambayo ameishi ni kumdhalilisha IGP.
“Matukio haya ya uvamizi kutokea Chanika, eneo ambalo nimeishi kwa zaidi ya miaka 28, ni kumdhalilisha IGP”
“Vijana wanaofanya haya matukio, wanakunywa pombe na kuvuta bangi, na wanatoka Kariakoo, Mbagala na maeneo mengine” amesisitiza IGP Sirro