
Jimmy Butler ameiongoza Miami kushinda game 5 dhidi ya Philadephia 76ers Amefunga alama 23
Ukanda wa Mashariki Miami Heat wameshinda mchezo wa 5 (game 5) leo Alfajiri dhidi ya Philadephia 76ers kwa alama 120 kwa 85 na sasa Miami wanaongoza kwa 3-2 kwenye mfululizo wa michezo 7 ya nusu fainali.
Katika mchezo huu mchezaji nyota wa Miami Jimmy Butler amefunga alama 23, pasi za kufunga (Assists) 6 na Rebound 6. Na Emmanuel Embiid wa 76ers hakuwa na game nzuri amefunga alama17 pasi za kufunga (Assist) 2 na Rebound 5.
Ukanda wa Magharibi mchezo wa 5 (game 5) ya nusu fainali Phoenix Suns wameinyuka Dallas Mavericks kwa alama 110 kwa 80. Nyota wa Suns Davin Booker amefunnga alama 28, pasi za kufunga (Assists) 2 na rebound 7. Luka Doncic wa Mavericks amefunga alama 28, pasi za kufunga (Assists) 2 na rebound 11. Mchezo wa 6 (Game 6) inachezwa kesho Mei 12, 2022.