Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

RC Malima aapa kupambana Mwekezaji apate leseni

Friday , 13th May , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema serikali ya mkoa kwa kushirikiana na Serikali Kuu, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  watafanya kila linalowezekana ili mwekezaji wa Kiwanda cha kuzalisha vilainishi na mafuta kwa ajili ya mashine na magari cha Mogas, kilichopo jijini Tanga

RC Malima ameyasema hayo wakati alipotembelea kiwanda hicho mara baada ya kupata malalamiko ya kukwamishwa kwa mwekezaji huyo katika upatikanaji wa leseni.

“Nataka nimhakikishie mwekezaji Mogas serikali itafanya kila linalowezekana ili apate leseni na kila anachohitaji kifanyike ili uwekezaji uende mara mbili. Sasa hao wanaokuja wanatoa taswira kwa watu wengine kwamba Tanga ipo kwa ajili yakupokea mitaji na uwekezaji na wanapeleka ujumbe mzuri kwa watu wengine na serikali ya mkoa tunawaunga mkono kwa asilimia 100" 

“Katika Mkoa wa Tanga nimeweka utaratibu wa kuhamasisha wawekezaji kushiriki na sisi moja kwa moja kwenye maendeleo ya serikali ya mkoa, kwa hiyo kama kuna mwekezaji amekuja ana jambo lake urasimu umekuwa mwingi tunataka kuviondoa hivyo"

“Leo kuna mwekezaji amekuja kufuatilia upatikanaji wa vibali akaambiwa asubiri miezi sita na sasa umepita mwezi mmoja na nusu, leo kaja kuniambia Mheshimiwa hatutaki kuwachongea lakini miezi sita kweli, na hicho kibali chenyewe mimi nauliza ni cha kusaini kwa mkono sasa kusaini kwa mkono miezi sita"

“Kwa hiyo sasa hawa wenye matendo ambayo mimi nawaita ya kipuuzi kumzuia mwekezaji ambaye amekuja nchini kwako kwa lengo la kuleta mitaji na mambo mengine, uwekezaji ule ndiyo unaleta ajira za ziada na kodi hata mzunguko wa fedha,” amesema RC Malima. 

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Mogas, Geofrey Rugazoora alisema wanaishukuru serikali mkoani Tanga ambapo pia ameahidi kutoa mchango chanya katika kuchangia maendeleo mkoani hapa.

HABARI ZAIDI

Bashiri Mohamed (35) Mwenye Koti Jeusi akiwa anafikishwa Mahakamani Ilemela, Jijini Mwanza

Aliyezini na binti yake apandishwa kizimbani

Kamanda wa Polisi mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Agustino Senga

Polisi waambiwa kazi yao ni kazi ya Mungu

Kiwanda cha sukari Mtibwa

11 wafariki dunia kiwanda cha Mtibwa

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC Kapenjama ataka uaminifu kwa wakulima Songea

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Wanahabari wasisitizwa kuzingatia maadili ya kazi

Wilman Kapenjama Ndile, Mkuu wa Wilaya ya Songea

DC atangaza msako kuwaondoa walinzi wazee kazini