Thursday , 19th May , 2022

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera, John Joseph amesema wanafanya uchunguzi katika miradi 12 ya maendeleo, 

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Kagera, John Joseph

Amesema hatua hiyo inakuja baada ya kufanya ufuatiliaji wa miradi 28 yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 7.4 na kubaini kuwepo kwa kasoro katika baadhi ya miradi.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa kazi za taasisi hiyo katika kipindi cha miezi mitatu inayoanzia Januari 01 hadi Machi 31 mwaka huu, Mkuu huyo wa TAKUKURU amesema kuwa, ufuatiliaji huo ulifanyika katika ukarabati wa miradi ya Maji, Ujenzi wa Hospitali, vituo vya afya, Zahanati na ujenzi wa Madarasa, chini ya mpango wa maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19.