Tuesday , 24th May , 2022

Watu kumi wamepoteza maisha na wengine kujeruhuiwa baada ya jengo moja ambalo lilikua halijakamilika kuanguka huko kusini magharibi mwa   Iran

Vikosi vya uokoaji vinafanya kazi usiku na mchana ili kuwaokoa watu walionaswa kwenye mabaki ya jingo hilo.  

Mabaki ya kokoto na nondo yameanguka barabarani na kuangukia magari yaliyokua yameegeshwa.  

Uchuguzi juu ya kuanguka kwa ghorofa hilo unaendela. Baadhi ya watu  walionaswa kwenye jengo hilo saa za awali waliokolewa nna kukimbizwa hosptali .

Mmiliki wa jengo hilo tayari ametiwa nguvuni. Jengo hilo lilikua linajengwa kwenye mtaa wa  Abadan, mtaa ambao una harakati nyingi sana za kibiashara.   

Mashuhuda wamesema kuwa walihisi ni tetemeko la ardhi.