Saturday , 25th Jun , 2022

Nahodha wa Wales,Gareth Bale amekubali kujiunga na Klabu ya Los Angeles Fc akiwa mchezaji huru. Nyota huyo amejiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Marekani MLS baada ya Mkataba na Mabingwa wa Ulaya Klabu ya Real Madrid.

Gareth Bale akishangilia bao alipoifungia timu yake ya Taifa ya Wales.

Bale mwenye umri wa miaka 32 ameondoka Real Madrid baada ya kuitumikia kwa miaka 9 huku akijivunia kutwaa taji la Ligi ya mabingwa mara tano.

Nyota huyo alisajiliwa kwa ada ambayo ilishikilia rekodi ya dunia kipindi hicho cha mwaka 2015(Paundi Milioni 85) akitokea Tottenham Hotspurs.

Anajiunga na beki wa zamani wa Juventus Giorgio Chiellini ambaye amesajiliwa na Los Angeles FC mapema mwezi huu.