
Newcastle United, Chelsea na Manchester United zote zimeonyesha nia yakutaka kumsajili Neymar Jr
Klabu ya Manchester United ipo tayari kutoa dau la Euro milioni 60 kama ada ya uhamisho ya kiungo Frenkie de Jong kutoka FC Barcelona ambayo ni zaidi ya Bilioni 147 (147,712,230,341.48) kwa pesa ya Tanzania. Ripoti kutoka Hispania zinaripoti kuwa FC Barcelona wao wanataka dau la Euro milioni 80 ili waweze kumuuza mchezaji huyo ambayo ni zaidi ya Billion 196 kwa pesa ya Tanzania.
Taarifa Kutoka nchini Ufaransa zinaripoti kuwa mchezaji nyota wa PSG Neymar Jr yupo tayari kuondoka katika klabu hiyo katika dirisha hili la majira ya kiangazi 2022. Wiki kadhaa zilizopita iliwekwa wazi kuwa PSG wapo tayari kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazili mwenye umri wa miaka 30. Klabu za England Newcastle United, Chelsea na Manchester United zote zimeonyesha nia yakutaka kumsajili mshambuliaji huyo.
Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag amezuia nahodha wa klabu hiyo Harry Maguire asiondoke klabu hapo. Inaaripotiwa kuwa FC Barcelona ya Hispania inataka beki huyo raia wa England awe seheumu ya mabadirishano ya uhamisho ya kiungo Frenkie de Jong ambaye Manchester United wanataka kumsajili. Lakini kocha Ten Hag amegoma mpango huo na Manchester United wapo tayari kutoa ada ya uhamisho ambayo haitamuhusisha mchezaji huyo.
Na the Gunnars klabu ya Arsenal imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Gabriel Jesus kwa mkata wa miaka 5. Kwa mujibu wa ripoti Arsenal wamefikia makubaliano na mchezaji huyo raia wa Brazil na amekubali kusaini miaka 5. Awali iliripotiwa kuwa Arsenal na Manchester City zilifika makubaliano ya kufanya biashara ya mchezaji huyo na Arsenal watalipa dau la Pauni millioni 45 kama ada ya uhamisho ambayo ni zaidi bilioni kwa pesa ya Tanzania.
Washika bunduki wa London Arsenal wanafanya usajili wa mshambuliaji huyu baada ya washambuliaji wawili wa klabu hiyo Alexandre Lacazette na Piere Aubameyang kuondoka klabu hapo. Huu pia utakuwa usajili wa 4 kwa Arsenal baada ya usajili wa Fabio Vieira, Marquinhos na golikipa Matt Turner.