Tuesday , 28th Jun , 2022

Nyakasura ni shule ya mchanganyiko ya bweni, ya kati na upili iliyopo huko magharibi mwa nchi ya Uganda ambayo wanafunzi wa kiume wanavaa sare za 'Kilt' zenye muonekano wa sketi.

Picha za wanafunzi wakiwa wamevaa sare za Kilt

Unaambiwa shule hiyo ilianzishwa miaka 96 iliyopita na Missionary wa Scotland Kamanda Enest Calwell ambaye inasemekana ndio ameanzisha utamaduni wa kuvaa sare hizo.

Mkuu wa Shule hiyo amekanusha kwa kusema sare hizo za 'Kilt' sio sketi na huvaliwa kwa kawaida huko nyanda za juu Scotland.