Wednesday , 3rd Aug , 2022

Jumla ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) 36 wamechukua fomu za kuwania Ubunge wa Afrika Mashariki.

Wanachama hao ni kutoka maeneo matatu ambayo ni makao makuu ya CCM - Dodoma, Afisi Kuu ya CCM - Zanzibar na Ofisi Ndogo ya CCM-Dar es Salaam

Katibu Msaidizi Mkuu Idara ya Organaizesheni CCM, Solomoni Itunda  amesema kuwa wanachama 13 waliochukua fomu ni Jonas Lufungulo, Dk Linda Salekwa, Loti Lembrice, Richard Mbuguni, Angela Kiza, Mwansheria Pascal Mayala.

Wengine ni Francis Nanai, Melinda Muganda, Fikiri Luganga, Mkondo Fabian, Albert Mbago, Robison Etuttu na David Mwakanjuki.

Juzi, wanachama 23 waliochukua fomu kuwania nafasi hiyo ni Amani Kajuna, Azizi Mussa, Judith Mollel, Amedeus Mzee, Kalunde Malale na William Reuben.

Wengine ni Fancy Khuni, Salma Mwassa, Ngwaru Maghembe, Happyness Lugiko, Shabu Makonyola, Salimu Kungulilo, Prof Norman Sigalla, Harrison Lukosi, Rehema Hassan, Ahmed Nkhuli, Steven Mkomwa, Dorica Gwilenza na Ansar Kachabwa.

Aliongeza kuwa wengine ni Nadra Juma Mohamed, Ahmed Shehe Saleh, Mar-yam Said Mussa na Mourie Oscar Sendera.

Itunda alitoa wito kwa wanachama wengine wenye vigezo kuendelea kujitokeza kuchukua fomu ii kuwania nafasi hizo ikiwa ni kutimiza takwa la kikatiba.

Julai, 28 mwaka huu Chama cha Mapinduzi (CCM), kilitangaza kuanza kwa zoezi la uchukuaji wa fomu kwa ajili ya kugombea nafasi ya ubunge wa Afrika Mashariki ambapo zoezi hilo lilianza jana na linatarajiwa kukamilika Agosti 10,2022