
Kwenye hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hiyo vya kijeshi, waziri wa ulinzi nchini Mali Sadio Camara, amesifu msaada huo na kusema kuwa ni matunda mazuri ya mahusiano baina ya Mali na Russia.
Kwenye ukurasa wake wa Twitter Rais wa Mali alipost picha za vifaa hivyo muhimu vya kijeshi.
Mahusiano baoina ya nchi hizo mbili yamekua makubwa toka yalipotokea mapinduzi ya akijeshi mwezi may mwaka jana.
Ufaransa iliyaondoa majeshi yake nchini Mali baada ya nchi hiyo kuonekana kuanza kuwa karibu na Russia. Mashambulizi ya kijihad yamekua yakiongezeka katika wiki za hivi karibuni na kugharimu maisha ya watu.
Wikiendi iliyopita majeshi ya kijihad yaliwaua raia 17 wakiwemo wanajeshi.
Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa askari wengine 9 hawajulikani walipo huku 22 wakijeruhiwa