Wednesday , 10th Aug , 2022

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez “Chicharito” ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya LA Galaxy ya Marekani amesema yupo tayari kurejea Manchester United ili kusaidi kutatua changamoto ya eneo la ushambuliaji ambalo linaonekeana kuisumbua klabu hiyo kwa sasa.

Javier Hernandez 'Chicharito' yupo tayari kurejea Manchester United

Chicharito aliichezea Manchester United kwa misimu 6 kati ya msimu wa 2010-11 hadi 2014-15 ambapo alicheza michezo 157 na alifanikiwa kufunga magoli 59, akiwa na The Red Devils ameshinda makombe 4 ikiwemo ubingwa wa Ligi Kuu England EPL mara 2.

Chicharito amesema kama atapata ofa ya usajili kutoka Manchester United yupo tayari kujiunga na klabu yake hiyo ya zamani.

"Ikiwa United watakuja kwangu nitasema ndiyo, nitacheza bure.' bila shaka, unajua, nitafanya hivyo. pia nataka kuwa na heshima kubwa kwa klabu yangu la Galaxy’’. Amesema Chicharito

Mshambuliaji huyo raia wa Mexico amesema hayo kufuatia Manchester United kuwa na mahitaji kwenye eneo la ushambuliaji kufuatia kuumia kwa Antony Martial lakini pia Christiano Ronaldo anataka kuondoka klabu hapo hivyo kocha Erik ten Hag anahitaji kuongeza nguvu, na wachezaji Benjamin Sesko na Marko Arnautovic wote wanahusishwa kujiunga na klabu hiyo.