Sunday , 28th Aug , 2022

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka, ametangaza mkoa wake kukamilisha zoezi la kuhesabu watu katika dodoso kuu na maeneo yote na kinachoendelea sasa ni zoezi la kuhesabu makazi kwenye Sensa ya Watu na Makazi kwa mwaka huu. 

Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka

Akitangaza kukamilika kwa zoezi hilo akiwa Tandala Ikonda wilayani Makete, RC Mtaka, amesema makarani na viongozi mbalimbali wameshirikiana vyema katika utekelezaji wa zoezi hilo na kwamba kinachoendelea sasa ni Dodoso la Makazi. 

Awali mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda amesema wilaya yake imevuka lengo la makadirio ya uhesabuji watu katika kaya zao jambo ambalo limeonesha mafanikio makubwa ya sensa ya mwaka huu. 

Akitoa taarifa ya ukamilishaji wa zoezi hilo Mratibu wa sensa wilaya ya Makete Bwana Aloyce Mwalukisa amesema wamefikia asilimia 113 katika uhesabuji watu ndani ya wilaya yao.