Monday , 29th Aug , 2022

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda amesema hadi kufikia saa mbili asubuhi ya leo kaya zilizohesabiwa ni asilimia 93.45 na hivyo wameamua kuongeza muda wa ziada wa siku 7 kukamilisha zoezi hilo

Kamisaa wa sensa ya watu na makazi Anna Makinda

Makinda amesema katika siku hizo mwananchi ambaye hajahesabiwa atapatiwa namba ya simu ambayo atapiga na kutoa taarifa zake kuanzia kesho

Amewataka wananchi ambao hawajahesabiwa  katika zoezi hilo kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaokuwa wanazungumza nao kwa njia ya simu ili  kutoa taarifa zao

Katika hatua nyingine Kamisaa huyo wa sensa ya watu na makazi ametangaza kuanza sensa ya majengo nchi nzima ambayo itaanza mara tu baada ya kukamilika kwa zoezi la sensa ya  watu na makazi

Akizungumzia changamoto zilizojitikeza wakati wa zoezi hilo ikiwemo vishkwambi kuisha umeme na baadhi ya makarani na wajumbe wa mtaa kutolipwa posho zao mkurugenzi wa huduma za sensa amesema hakuna mtu ambaye hatalipwa