Tuesday , 30th Aug , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amesema mpaka asubuhi ya leo Agosti 30/2022 zaidi ya asilimia 94.3 ya wananchi wa jiji hilo wamehesabiwa

Akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya mwenendo wa zoezi hilo kwa mkoa, RC Makalla amesema Makarani ambao bado hawajakamilisha kutuma taarifa wakituma taarifa zote ni dhahiri kuwa Mkoa utakuwa umefikia Asilimia 100

Aidha RC Makalla amesema mkoa huo unafanya zoezi hilo kwa umakini mkubwa ili kupata takwimu sahihi na za uhakika kutokana na mkoa huo kuchukuwa asilimia 10-13 ya Wananchi wote wa Tanzania

Ili kuhakikisha kila mmoja anahesabiwa, RC Makalla amewataka Wananchi ambao bado hawajahesabiwa kufika Ofisi ya Serikali ya mtaa na kuacha mawasiliano au kupiga simu kupitia namba maalumu zilizotangazwa kwa kila wilaya ili aweze kufikiwa

Pamoja na hayo RC Makalla amempongeza Kamisaa wa Sensa Anna Makinda kwa kuongeza siku ambapo pia amewapongeza Wakuu wa Wilaya kwa kusimamia Vizuri zoezi Hilo.