
Chanjo ya Polio
Mganga mkuu wa mkoa huo, Dkt. Khery Kagya, ameyaeleza hayo katika kikao kazi cha msingi juu ya kampeni hiyo na kusema chanjo hiyo awamu ya tatu, itakuwa ya siku nne, kuanzia Septemba Mosi hadi 4 mwaka huu na itahusisha na watoto walio kwisha kupewa awamu ya pili,lengo likiwa ni kuzuia kuenea kwa ugonjwa huo hapa nchini.
Dkt. Kagya, amesema chanjo hiyo ya matone ni mwendelezo chanjo ya Polio iliyotolewa awamu ya pili ya mlipuko wa ugonjwa huo,uliotokea nchi jirani za Malawi na Msumbiji miaka mingi iliyopita
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Lindi, Zainabu Telack, akizungumza na wajumbe katika kikao kazi hicho, amesema ni muhimu kuwapa watoto kinga, huku akiwaomba wazazi na walezi kuhakikisha wanatoa ushirikiano na wataalamu wa afya kuwakinga watoto wao.