
Kikosi chetu cha Simba Queens
Simba Queens imepata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika nchini Morocco.
Wekundu hao ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) kwa misimu mitatu mfululizo, waliweka heshima na kuandika rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kutwaa taji la Cecafa baada ya kuifunga She Corporates ya Uganda.
Simba kwa kubeba ubingwa huo sasa itashiriki Ligi ya Afrika itakayofanyika Oktoba, mwaka huu itakayoshirikisha timu nane wakiwamo mabingwa watetezi Mamelodi na mwenyeji Far Rabat.
Akizungumza na waandishi wa habari kocha Nkoma amesema amefurahishwa kutwaa taji hilo na kuwa miongoni mwa timu zilizoleta msisimko wa mpira, lakini bado ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na upungufu aliouona.
“Yalikuwa mashindano mazuri kwetu, yametujengea kujiamini na yametoa kipimo kikubwa kuelekea mashindano ya kimataifa. Nina kazi ya kufanya kwa sabau kuna upungufu nimeuona,” amesema kocha huyo.