
Caroline Garcia ameshinda michezo 13 mfululizo
Carolina amemfunga Gauff kwa seti mbili mfululizo 6-3 na 6-4 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Arthur Ashe. Raia huyo wa ufaransa ambaye anashika nafasi ya 17 kwenye viwango vya ubora kwa wanawake amekuwa kwenye kiwango bora kwani huu ni mchezo wake wa 13 mfululizo ameshinda.
Na katika hatua hiyo ya nusu fainali atacheza dhidi ya mtunisia Ons Jabeur ambaye amefuzu kucheza katika hatua hiyo baada ya kumfunga Ajla Tomlijanovic na kuweka rekodi yakuwa mwanamke wa kwanza kutoka Afrika kufuzu hatua ya nusu fainali.