Wednesday , 21st Sep , 2022

Wakala wa Majisafi na Usafi wa Mazingia Vijijini (RUWASA) mkoa wa Rukwa, imefanikisha upatikanaji wa majisafi na salama karibu na na wananchi kufuatia kukamilika kwa mradi wa maji wa Kijiji cha Kalaela wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa utakaohudumia wakazi 3,588.

Tenki la maji wilayani Kalambo

Akizungumza kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi mradi wa maji  katika Kijiji hicho kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Geraruma, aliwapongeza RUWASA kwa kujenga mradi huo kwa ubora na kuwataka wahakikishe miundombinu iliyojengwa inakuwa imara na kuepusha maji kuvuja.

Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa RUWASA wilaya ya Kalambo Mhandisi Patrick Ndimbo alisema jumla ya shilingi milioni 152.5 kati ya shilingi milioni 436.5 zimetumika kujenga mradi unaotekelezwa kupitia fedha za maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19. 

Katika hatua nyingine Mwenge wa Uhuru umezindua mradi wa ujenzi vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari Mwazye uliogharimu shilingi milioni 80.