
Sababu za nyangumi hao kukwama hazijajulikana ambapo kundi la waokozi limetumwa eneo hilo ili kusaidia kuokoa maisha yao . Tukio hilo linajiri katika kipindi ambacho ni siku moja tu tangu kukwama kwa nyangumi wengine huko kaskazini mwa Tasmania. Tukio hilo la jumanne wiki hii limeshuhudia vifo vya nyangumi 14 .
Wanyama hao jamii ya mamalia hujikuta wamepata madhara kwa pamoja sababu ya tabia yao ya kusafiri kwa pamoja kwenye kundi kubwa . Mwaka 2020 nyangumi takribani 500 waliokolewa baada ya kukwama kwenye eneo hilo. Mtaalamu wa wanyama hao amesema kuwa sababu zinaweza kuwa kiongozi wa msafara wa nyangumi kuumwa na kupelekea msafara kusimama, ama msafara kuelekea uelekeo usio sahihi kwenye maji machache.