Wednesday , 12th Oct , 2022

Mwenyekiti wa Bodi ya Amref Afrika nchini Tanzania amesema kwamba taasisi hiyo inajitahidi kufanya kazi na wadau wake ili kupunguza vifo vya wanawake wanaofariki kutokana na matatizo wakati wa kujifungua.

Mjamzito

Ni nje ya mkutano uliowakutanisha shirika la Amref Africa na washikadau wake muhimu ikiwemo kampuni ya IPP ambapo katika mahojiano na EATV, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi, Amref Africa nchini Tanzania Bw. Anthony Chamungwana anataja hali ya vifo vya wanawake wanaojifungua na ni kipi wanakifanya kumaliza hali hii.

“Amref Afrika hapa Tanzania tumekuwa tukifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wadau wetu mhimu ili kupunguza vifo kwa wanawake wanaojifungua, mfano ukiangalia kwa takwimu za afya mwaka 2015/2016 zinaonesha kwamba wanawake 500 hadi 600 hufariki kati ya wanawake laki moja wanaojifungua. Kwahiyo kukutana  na wadau wetu ni kuongeza mashirikiano na kuona namna bora ya kuendelea kushirikiana kusaidia katika afya hasa wanawake, afya ya mabinti na wanawake wanaojifungua"- Anthony Chamungwana, M/kiti bodi ya wakurugenzi Amref Africa Tz.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano wa IPP Media Nancy Mwanyika ambaye pia ameshiriki katika hafla hiyo ya washikadau, amesema namna wanavyoshirikiana na Amref katika kuisaidia jamii.