
Mashirika ya kiraia yaliyoandaa maandamano hayo yalimshutumu waziri wa kilimo kwa kuruhusu raia wa kigeni kujihusisha na biashara ya punda. Kwa sasa Muswada wa sheria ya kudhibiti biashara ya punda kwa sasa unachukua nafasi kwenye bunge la nchi hiyo.
Mwezi uliopita,mamlaka za huduma ya forodha Nigeria zilikamata sehemu za siri za punda dume wapatao 7,000 katika uwanja wa ndege katika kitovu cha kibiashara, Lagos, ambao ambazo zilikua zikisafirishwa nchini China.
Sehemu za punda zinahitajika sana nchini China kwa matumizi ya dawa za kienyeji.