
Kauli ya John Mnyika ameitoa leo wakati akizungumzia ripoti ya kikosi kazi kilichoundwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo moja kati ya mambo yaliyoibuliwa ni suala la mikutano ya kisiasa ya hadhara
"Mikutano ya hadhara zuio haramu liondolewe, kwa kauli ya Rais bila kusubiri marekebisho ya kanuni na sheria, na wakati kauli hiyo ikisubiriwa ngazi zote za chama ziendelee na maandalizi ya mikutano ya hadhara"
Rais wa Tanzania akipokea ripoti hiyo ya kikosi kazi jana Aktoba 21 alisema suala la mikutano ya hadhara linahitaji kutupiwa jicho kanuni zake za mwaka 2019 ili kuondoa madhara yanayoweza kujitokeza