Saturday , 22nd Oct , 2022

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limesema halitaruhusu mtu yeyote kwenda na silaha ya aina yoyote kesho uwanjani kwenye mechi ya Simba na Yanga isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la kulinda usalama eneo hilo. 

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro,

Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 22, 2022, na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo Jumanne Muliro, na kusema kuwa jeshi hilo linachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo na kwamba usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu ili kuwezesha mchezo huo kufanyika kwa amani.

Kamanda Muliro amezitaja silaha zilizozuiliwa kuingia nazo uwanjani ni pamoja na silaha za moto kama vile bunduki, bastola na milipuko ya aina zote, silaha zenye ncha kali kama vile mapanga, visu, mikuki, mishale, nyembe na bisibisi, silaha butu kama vile nyundo, nondo, kipande cha chuma, na silaha za jadi kama vile fimbo, marungu na mawe.