Sunday , 23rd Oct , 2022

  Ikulu ya Kremlin imesema kwamba , Rais wa Urusi Vladimir Putin ametuma ujumbe wa pongezi kwa Rais wa China  Xi kwa muhula wake wa tatu.

Xi Jinping amechaguliwa tena kuwa katibu wa chama kwa muhula wa tatu mfululizo katika historia ya nchi hiyo.

Putin alimwambia Xi kuwa anatarajia kuendeleza zaidi "uhusiano wa kina" kati ya nchi hizo mbili.

Washirika hao walikutana mara ya mwisho katika mkutano wa kilele wa Shirika la Ushirikiano wa Shanghai nchini Kazakhstan ambapo walifanya mkutano wa moja kwa moja kuthibitisha uhusiano wao.

Mwezi Februari nchi hizo mbili zilitangaza urafiki usio na "mipaka" na "hakuna maeneo yaliyokatazwa ya ushirikiano"  muda mfupi kabla ya Urusi kuivamia Ukraine.