Monday , 24th Oct , 2022

Uhifadhi wa misitu ya asili hasa  aina ya miti ambayo imekuwa ikitumika kama dawa iko hatarini kutoweka kabisa kutoka na na shughuli nyingi za binadamu ambazo zimekuwa zikipelekea  miti hiyo kuteketezwa pasipo kuendelezwa.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Levocatus Mshumbusi,

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Levocatus Mshumbusi, wakati wakiendesha kikao kazi na watalaam wa tiba za asili mkoani Tabora na kusisitiza kuwa miti  ya dawa katika misitu kwa sasa ipo kwa 25% tu ukilinganisha na ukubwa wa mahitaji .

Amesema ukiachilia mbali na shughuli zingine za kibinadamu kama kilimo ambazo zimekuwa ni sababu ya kuteketea kwa miti dawa, pia kumekuwepo na aina ya uvunaji mbaya wa kuua miti kabisa kwa kubandua magome na kuchimbua kwa kukata mizizi yake.

Aidha ametaja kuna kila sababu ya kuwekwa mazingira ya uhifadhi wa miti dawa kutokana na umuhimu wake wa kutumika kama dawa kwa faida sasa na vizazi vijavyo.