Monday , 31st Oct , 2022

Serikali imeshauriwa kueleza mikakati itakayotumiwa kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na bima ya afya  bila kuhusisha matumizi ya nguvu ikipendekezwa kanuni zieleze wazi na zifanyiwe mapendekezo na kamati ya kudumu ya bunge ya sheria ndogo ili kuondoa malalamiko ambayo yamekuwa yakitokea

Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC)wakili Anna Henga

Utakumbuka september mwaka huu kabla ya bunge kuhahirishwa tarehe 23,2022 pamoja na mambo mengine ilisomwa miswada minne kwa mara ya kwanza ukiwemo ule wa bima ya afya kwa wote,mswada wa sheria ya uwekezaji,ulinzi wa taarifa binafsi pamoja na maboresho ya sheria mbalimbali na kuruhusiwa wadau kutoa maoni yao ambapo Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu wakili Anna Henga amesema kabla ya utekelezaji serikali itumie maoni iliyopokea ya wadauili kuja na majibu.

Amesema yapo maeneo ambayo muswada umebainisha kuwa endapo mtu atakosa kadi ya bima ya afya basi atashindwa kupata huduma nyinginezo ikiwemo kitambulisho cha taifa,leseni ya udereva,leseni ya biashara,huduma ya usajili wa laini za simu hali ambayo ni kinyume na haki za binadamu hivyo kuitaka serikali kueleza kwa namna gani hali ilivyo.

Aidha wito umetolewa kwa serikali kuvitazama upya vifungu vyote vinavyompa mamlaka wazirir mwenye dhamana ya afya kutunga kanuni ili kuondoa uwezekano wa kukinzana na sheria mama na baadhi ya sheria baada ya kupitishwa na bunge.