Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana
Akiwa katika hifadhi hiyo Waziri Balozi Dkt. Chana amepokea taarifa ya utekelezaji wa kazi inayoendelea ya kuzima moto akiwashukuru na kuwapongeza wadau wote waliojitolea kwa hali na mali katika kuhakikisha moto unadhibitiwa katika maeneo yote.
Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana ameendelea kukemea vikali tabia ya baadhi ya wananchi wanaoanzisha au kuchoma moto hovyo katika maeneo yaliyohifadhiwa na kuisababishia serikali na wananchi wake hasara kubwa, na kusisitiza kuwa yeyote atakayebainika atafikishwa kwenye vyombo vya sheria.