
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa Allan Bukumbi amesema jithada hizo za kukamata majangili ni kutokana na msako wa jeshi hilo kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya taifa ya Ruaha
Kwa upande wake Kamanda wa uhifadhi nyanda za juu Kusini Joas Makwati amesema meno hayo ya tembo ni ya muda mrefu na yalikuwa yamehifadhiwa na majangili hayo kwa ajili ya kutafuta wateja
Katika hatua nyingine jeshi hilo limefanikiwa kupata silaha 13 ikiwa ni mafanikio ya zoezi la kusalimisha silaha lilioendeshwa katika maeneo mbalimbali