Friday , 4th Nov , 2022

Familia ya watu 15 wakazi wa Kijiji cha Kinango Kata ya Nyigogo wilayani Magu mkoani Mwanza, imelazimika kulala chini ya mti wa mwembe baada ya kubomolewa nyumba waliyokuwa wakiishi kutokana na mgogoro wa ardhi.

Familio iliyobomelewa nyumba

Tukio la kubomoa nyumba hiyo limetokea Oktoba 25, 2022, baada ya Suzana Maige, anayedai kupewa ardhi hiyo kwa amri ya Mahakama na kubomoa nyumba hiyo hivyo familia hiyo kubaki bila makazi na kuamua kuhamishia makazi yao chini ya mwembe uliopo ndani ya shamba hilo.

"Nilinunua ardhi hii mwaka 1981 aliyeniuzia ameshafariki ndipo akaibuka mwanae na kudai kuwa ni ardhi yake na kunitaka niondoke, baada ya mvutano mrefu nilifungua kesi katika Mahakama ya Mwanzo Magu nikatakiwa kutoa hela ili shauri langu lifanyiwe kazi lakini nilikuwa sina hela," ameeleza Ikoma Njige ambaye ni mkuu wa familia

James Rafael ni mwenyekiti wa Kijiji cha Kinango amesema baada ya kupokea taarifa hizo aliwaandikia barua ya kwenda kwa mkuu wa wilaya ya Magu ili kupata ufafanuzi wa suala hilo, kwani familia hiyo inateseka kwa watoto kukosa chakula na wengine kushindwa kwenda shule.