Friday , 4th Nov , 2022

Serikali ya China imetoa mkopo wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 56.72 wenye masharti nafuu kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar, Terminal II

Taarifa ya Ikulu ya Tanzania imeeleza kuwa pia China imeipunguzia Tanzania sehemu ya deni lake la thamani ya Shilingi Bilioni 31.4

Rais Samia yupo nchini China kwa ziara ya Kiserikali kufuatia mwaliko kutoka kwa Rais wa nchi hiyo ambapo pia alikutana na kuzungumza na Waziri Mkuu wa China pamoja na Spika wa Bunge la nchi hiyo

Katika ziara hiyo Rais Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais wa China Xi Jinping wameshuhudia utiaji saini wa Mikataba na Hati za Makubaliano ya kimkakati 15