Monday , 21st Nov , 2022

Vijana Zaidi ya mia mbili jijini Mwanza wamepewa mafunzo ya kuhamasisha jamii kupanda na kutunza miti ikiwa ni lengo kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutunza mazingira 

Mafunzo hayo kwa vijana ziaid ya mia mbili yametolewa na shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na utunzaji wa mazingira la ECOFA ambapo katibu wa shirika hilo Thomas Mponeja amesema kumekuwa na uharibifu mkubwa wa mazingira hivyo wakaona ipo haja ya kutoa mafunzo hayo ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

"Wao wametuahidi wataweza kuitengeneza dunia yetu kuwa ya kijani wataanza na familia zao wametuahidi watapanda miti watakata mti mmoja na kupanda miti mizuri tutawafatilia kila kaya na kila kikundi"

‘Wamejiajiri kwa njia hiyo kwa kuboresha mazingira bila kujali kwamba mimi niwe na kazi Fulani wanacheza na udongo unaweza kudhani hawana kazi za kufanya kumbe wanahamasisha utunzaji wa mazingira

Kwa upande wao baadhi ya vijana walioshiriki mafunzo hayo wamesema wataitumia vyema elimu waliyoipata katika kuwahamasisha wenzao na jamii kwa ujumla kutunza na kuhifadhi mazingira.

"Kiukweli tumejifunza mambo mengi sana ambayo mimi kama kijana yametia moyo ya kuweza kuwahamasisha vijana wenzagu katika utunzaji wa miti yetu"