Monday , 28th Nov , 2022

Serikali Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa imeombwa kutoa mafunzo zaidi kwa wanawake katika jamii yanayohusu utoaji huduma za afya ngazi ya jamii ili kukabiliana na matatizo yatokanayo na upungufu wa Lishe.

Wanawake wa Wilaya ya Nkasi

Hali hiyo itasaidia Jamii kuwa na uelewa zaidi wa kuzingatia lishe bora kwa watoto na kuwaepusha watoto dhidi ya Utapiamlo ambao unatajwa kuendelea kuonekana kwa watoto katika Mkoa wa Rukwa.

Dr Martha Chacha ambaye ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi amesema uhaba wa watoa huduma ngazi ya jamii kwenye vijiji unachangia wanajamii kukosa elimu juu ya kuzingatia lishe kwa watoto wao hivyo ni muhimu kuhakikisha katika jamii watoa huduma za afya ngazi ya jamii kuongezeka.

Aidha katika hatua nyingine wanafunzi wameomba kuhakikisha shule zinazotoa huduma ya chakula shuleni wanazingatia Lishe ili kuwaepusha na udumavu.