Mastaa wa timu zilizofuzu hatua ya Robo Fainali Kombe la Dunia 2022
England itapambana na Ufaransa, timu hizi zitakutana kwa mara ya 3 kwenye fainali za Kombe la Dunia ambapo kwenye michezo 2 iliyopita yote England ilishinda. Mwaka 1966 waliinyuka Ufaransa mabao 2-0 na 1982 walishinda mabao 3-1. Huu pia utakuwa mchezo wa 32 timu hizi zinakutana kwenye mashindano yote, England wameshinda mara 17 sare michezo 5 na Ufaransa wameshinda mara 9.
Argentina watapambana na Uholanzi, ambapo rekodi zinaonesha timu hizi zimekutana mara 5 kwenye Kombe la Dunia. Uholanzi wameshinda mara 2, Argentina wakishinda mara moja na mara 2 wakitoka sare. Mara ya mwisho timu hizi kukutana kwenye Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 2014 hatua ya Nusu Fainali nchini Brazil ambapo Argentina ilishinda kwa mikwaju ya penati 4-2.
Mchezo mwingine ni Croatia dhidi ya Brazil. Croatia hawajawahi kuifunga Brazil kwenye michezo minne waliyokutana. Wamefungwa mara 3 na wametoka sare mchezo mmoja, Neymar Jr ndiye mchezaji wa Brazil anayeongoza kuifunga Croatia akiwafunga mabao matatu.