Sunday , 11th Dec , 2022

Shirikisho la soka Duniani FIFA limetambulisha mpira rasmi utakaotumika kuanzia hatua ya Nusu Fainali hadi fainali ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Qatar unaojulikana kama 'Al Hilm' ikimaanisha ndoto.

Mpira rasmi utakaotumika kwenye Nusu Fainali na Fainali Kombe la Dunia 2022

Michezo ya hatua ya Nusu Fainali itaanza kuanzia Disemba 13 ambapo Argentina itapambana na Croatia na Disemba 14 Ufaransa itapambana na Morocco.

Mpira rasmi uliokuwa ukitumia kwenye hatua ya makundi hadi Robo Fainali ulikuwa ukutambulika kama 'Al Rihla' ikimaanisha safari.