Monday , 12th Dec , 2022

Droo ya upangaji wa makundi wa Ligi ya mabingwa barani Afrika umekamilika nchin Cairo ambapo timu ya Simba kutoka Tanzania imepangwa kundi C

Katika kundi hilo Klabu ya Simba imepangwa na miamba ya soka barani Afrika  Raja Casablanca ya Morocco, Horoya ya Guinea pamoja na Vipers kutoka Uganda.huku mechi hizo zote zianzaa kutimua vumbi Mechi za hatua ya makundi zitaanza kupigwa kati ya Februari 10 hadi Aprili Mosi mwaka 2023 .

Simba ilifanikiwa kuingia katika Hatua ya Makundi katika mashindano ya Klabu Bingwa na sasa itakuwa na kazi ya kupambana na miamba hiyo, ili kusonga mbele.

Kazi kubwa kwa wawakilishi hao ni kusaka pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza jambo litakalowapa tiketi ya kusonga mbele.

Chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda timu hiyo ilifanikiwa kutinga hatua ya makundi jambo ambalo lilikuwa kwenye mipango ya Simba.

Awali droo hiyo ilipangwa kufanyika Jumatano ya Novemba 16 na sasa kufanyika leo kuanzia saa 8 mchana ikitanguliwa na ile ya Ligi ya Mabingwa yenye vigogo vitupu kabla ya mechi za hatua hiyo kuanza kupigwa Februari mwakani.