
Waziri Gwajima amekutana na wananchi wa Kata ya Kirongwe alipotembelea eneo hilo kukagua uundwaji wa Kamati za kupambana na ukatili wa wananwake na watoto wilayani Mafia
Waziri huyo ameonesha kutoridhishwa na uhai Mabaraza ya Watoto na Kamati za MTAKUWWA hasa kwenye ngazi za Vijiji na Kata, ambapo ameahidi kurudi wilayani Mafia na kupiga kambi ili aweze kuwafikia hadi wananchi walio katika visiwa vingine vidogo vidogo vinavyounda wilaya hiyo
Awali, Dkt. Gwajima alipokea taarifa kuwa matukio yanayoongoza kwa wilaya ya Mafia ni; ubakaji, ulawiti, mimba za utotoni na mashambulio ya aibu
Kwa Mwaka 2021/2022 Jumla ya matukio 493 yalitolewa taarifa katika Ofisi za Ustawi wa Jamii na kituo cha Polisi ambapo matukio 56 yalikuwa ya ubakaji na ulawiti, kutelekezwa 64, shambulio la mwili 134 na shambulio la aibu matukio 239
Kati ya kesi hizo zilizotolewa taarifa, kesi 53 zipo Mahakamani na kesi 4 wahusika wamefungwa ambapo mmoja amefungwa maisha, kesi 5 wapo katika kifungo cha nje, kesi 11 zimekosa ushahidi na kesi 9 zinaendelea.