Monday , 19th Dec , 2022

Jeshi la polisi Mkoani Mtwara linamshiklia mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Sinde  Kata ya  Msangamkuu, halmashauri ya Mtwara,  kwa tuhuma za kumnyonga mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili na nusu

Baadhi ya majirani wanasema mama huyo alimnyonga mtoto wake huku yeye na mtoto wakiwa uchi na kukimbilia porini ndio majirani walipomkimbiza na kumchukua mtoto lakini alikuwa tayari amefariki

Kaimu Kamanda jeshi  la polisi  Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo amesema mtuhumiwa atafikishwa mahakamani pindi uchunguzi utakapokamilika