Thursday , 22nd Dec , 2022

Kundi la Taliban, ambalo lilianza kama kundi la wapiganaji wa Kiislamu lenye msimamo mkali, liliahidi kuheshimu haki za wanawake waliporejea madarakani mwezi Agosti mwaka jana - baada ya kusitisha utawala uliokuepo, wao awali walitawala kutoka mwaka 1996-2001 wakati wanawake hawakuweza.

Lakini amri yao ya hivi karibuni inaondoa uhuru na haki ndogo zozote walizopewa wanawake baada ya majeshi yanayoongozwa na Marekani kuondoka Afghanistan na Taliban kurejea. miezi mitatu tu iliyopita, Taliban walikuwa wamekubali kuruhusu mitihani ya kujiunga na chuo kikuu kuendelea.

Maelfu ya wasichana na wanawake walifanya majaribio katika majimbo kote nchini. Wengi walikuwa wamesoma kwa siri - nyumbani au kuhatarisha kujitosa kwenye vyuo vya ualimu vilivyofichwa vilivyowekwa kwa ajili ya wasichana.

Hatari ilikuwepo kila wakati. Wakati baadhi ya mitihani washambuliaji walilenga shule na kuua wanafunzi.Lakini bado wasichana waliendelea kusoma.

Hata wakati Taliban mwezi Novemba walipoleta vikwazo vya dakika za mwisho kwa masomo - kuwazuia wasichana kutoka katika masomo kama vile uchumi, uhandisi na uandishi wa habari - waliendelea kujaribu, wengi wakiomba kufundisha na udaktari.