
Akizungumza wakati wa kongamano la wanawake katika manispaa ya Bukoba ambalo lilikwenda sambamba na uchangiaji damu, mratibu wa kitengo cha damu salama mkoa wa Kagera Dk. Boniphace Meza amewahasa wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao, ili kama wana maambukizi ya magonjwa mengine waweze kuyabaini na kupatiwa tiba.
"Kwenye jamii tunaweza kutoa damu nyingi lakini idadi ikapungua kutokana na nyingine kukutwa na maambukizi ya magonjwa, lakini katika shule wanachangia kwa usalama mkubwa kwa sababu tunaweza kutoa damu wanafunzi 200 majibu yakirudi mengi yanakuwa salama" amesema Dk. Meza.
Nao baadhi ya wachangiaji wamewataka wananchi wenzao kuacha woga na kujitokeza kuchangia damu, maana hakuna madhara yatakayowapata kama wengine wanavyodhani.
"Maana asilimia kubwa wanaogopa, wapo wanaofikiri kwamba kuna matatizo labda wakitolewa damu watakufa, lakini kutolewa damu ni hali tu ya kawaida tumethibitisha hilo kwa hiyo tunawasihi hata wanawake wenzetu wajitokeze" wamesema.
Kwa mujibu wa mratibu huyo wa damu mkoa wa Kagera, hali ya upatikanaji wa damu salama ni nzuri, kutokana na wananchi kuwa na mwamko wa kujitokeza kuchangia damu, maana kwa mwezi wanatumia kati ya chupa 180 hadi 200 ambazo kwa sasa zipo