Wednesday , 18th Jan , 2023

Rais wa Kenya William Ruto amesema katika uchaguzi uliomalizika mwaka jana 2022 kulikuwa na njama za moja kwa moja za kutaka kumteka nyara na kumuua mkuu wa tume ya uchaguzi Wafula Chebukati 

Ruto ambaye alitangazwa mshindi katika uchaguzi huo amesema njama hizo  zilipangwa baada ya kumalizika uchaguzi na kabla matokeo hayajatangazwa

"Tunajua kuwa kulikuwa na jaribio la moja kwa moja la kumteka nyara Bw Chebukati na kumuua ili tume isiweze kutekeleza kazi yake, au kamishna aliyetii sheria achukue mamlaka na kupotosha mamlaka ya watu. Ilikuwa wakati mgumu, baridi na upweke, vitisho vilikuwa vikali., zawadi zilizoahidiwa ni nyingi na shinikizo lisilokoma,” Rais Ruto alisema.

Aidha aliyekuwa mpinzani wake katika uchaguzi huo Raila Odinga, amesema tuhuma hizo hazina ukweli huku akitaka madai hayo yawasilishwe kwenye jopo la uchunguzi ili ukweli ujulikane