Thursday , 9th Feb , 2023

Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA imesema kuwa mvua zilizoanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zitaendelea kwa kipindi cha wiki mbili 

Mchambuzi wa hali ya hewa kutoka Mamlaka hiyo Rose Senyagwa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari

Mvua zilioanza kunyesha jana jijijini Dar es salaam zimeleta adha kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam ikiwemo foleni pamoja na baadhi ya vyombo vya usafiri kama  bajaji na pikipiki kuharibika kutokana na kuingia maji ambayo yamejaa kwenye baadhi ya barabara ikiwemo ile ya makutano ya jangwani.

Wakizungumza leo jijini Dar es salaam baadhi ya maderrva wa vyombo hivyo hasa pikipiki wameiomba serikali kuharakisha ujenzi wa daraja la jangwani ili liwe mkombozi kutokana na sehemu hiyo kuwa korofi.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wamelalamikia mto msimbazi kuto safishwa na kuwa chanzo cha maji kujaa barabarani kutokana na mto huo kujaa uchafu ulioziba njia ya mto huo.

Hayo yanajiri wakati serikali ikiwa katika mchakato wa ujenzi wa daraja la jangwani kupitia mkopo nafuu kutoka benki ya dunia ambalo ni takribani shilngi trilioni 1.24 ambapo daraja hilo litakuwa na urefu wa mita 300 kwenda juu  upanuzi wa mto kwa kilometa 1.8 kwenda juu .na kilometa 1.8 kushuka chini sanjari na kingo za zege  ili kutatua changanoto ya maji kujaa eneo la jangwani pindi mvua inapo nyesha .