Akizungumza na wanahabari rais huyo amedai kuwa makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front (TPLF) yaliharakishwa na Marekani ili kuwazuia waasi hao kushindwa katika uwanja wa mapambano.
Makubaliano ya amani yaliyotiwa saini nchini Afrika Kusini mnamo Novemba 2022 yalimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka miwili ambavyo vilisababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha mamilioni wakihitaji msaada mkubwa wa kibinadamu.
Katika mahojiano hayo, Bw Isaias pia alikiri kwa mara ya kwanza kwamba mamia kwa maelfu ya watu walikufa katika mzozo huo, ingawa hakufafanua kuhusu majeruhi wa Eritrea
Wiki iliyopita, kiongozi huyo mstaafu alikanusha ripoti kwamba wanajeshi wa Eritrea walifanya uhalifu wa kivita katika nchi jirani ya Ethiopia ambako walikuwa wamepelekwa kupigana pamoja na wanajeshi wa shirikisho na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.

