
Watuhumiwa hao ambao ni Said Selemani, Bakari Saidi Na Selemani Hassani wote ni wakazi wa Kijiji cha Nanjilinji wilayani kilwa ambapo inaelezwa kuwa walikamatwa Machi 30.2023 katika eneo la Nakiu wilayani humo wakiwa na shehena ya meno ya Tembo 90.
Watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa ya kukutwa na meno ya Tembo pamoja na tuhuma ya kujihusisha katika uuzaji wa nyara hizo za serikali kinyume na sheria ya wanyamapori Nambari 5 ya mwaka 2009.