
Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbas
Kauli hiyo ameisema wakati akifunga semina ya waongoza utalii zaidi ya 1,200 iliyofanyika jijini Arusha ambapo pia amewakumbusha kwamba watafurahia matunda ya maono ya Rais Samia ya filamu ya Royal Tour iwapo watajiongeza, watajiimarisha na watatenda kazi kwa weledi badala ya kuwekeza katika 'uzabizabina na ukiroho papo'.
“Ninyi ni waongoza utalii na sio waondosha watalii, fanyeni kazi kitaalamu na kwa ukarimu wa juu sana na sio kuwaongezea 'stress' watalii mara unaweka vibomu kwa kueleza shida zako mara nini, msingi wa huduma yenu kwa watalii ni ukarimu sio vibomu," amesema Dkt Abbas.