
Na faini ya shilingi milioni 2 kwa baa zenye makosa mapya
Mkurugenzi mtendaji wa baraza hilo Dkt, Samuel Gwamaka amesema katika oparesheni inayoendelea NEMC imezifungia baa sugu na zile za makosa mapya ambapo katika jiji la Dar es salaam wilaya ya Ilala baa 25. Kinondoni baa 19 Kigamboni 22, Temeke 12.
Zoezi hilo pia limegusa baa 6 mkoani Dodoma na Mwanza baa 5 huku wamiliki wa baa hizo wakitakiwa kuandika barua za kukiri makosa pamoja na kutoa maelezo ya kutorudia kosa hilo
Aidha Dkt. Gwamaka amesema miongoni mwa baa zilizofingiwa moja wapo imeshtakiwa mahakamani kutokana na baa hiyo kuwa sugu sanjari na kukiuka sheria nyingine ikiwemo maagizo ya serikali huku akieleza serikalli haitosita kufuta leseni lakini pia kuchukua hatua dhidi ya nyumba za ibada zitakazo kutwa na makosa ya kelele kubwa .
EATV imezungumza na baadhi ya wamiliki wa baa zilizokutwa na makosa bapo licha ya kukiri makosa wameiomba serikali kupunguza adhabu kutokana na biashara kutokuwa nzuri kwa sasa huku wakisisitiza elimu kuendelea kutolewa ili kuongeza uelewa wa viwango stahiki vya sauti kwenye baa na majumba ya starehe